In memory: Imelda Malata

18th June 2020

We are deeply saddened to hear about the passing of Imelda Malata, a SAY Community Monitor from Iringa, Tanzania. Raleigh Tanzania and Raleigh International remembers Imelda and sends our condolences to her family and the community of Kinengembasi.

Tunasikitika kupata taarifa ya msiba wa Imelda Malata aliyekuwa Mfuatiliaji wa Jamii kupitia mradi wa Uwajibikaji wa Jamii Kupitia Vijana (SAY) huko Iringa, Tanzania. Raleigh Tanzania na Raleigh International tutamkumbuka Imelda na tunapenda kutuma salamu za rambirambi kwa familia ya Imelda na Kijiji cha Kinengembasi.

Swahili

Tunasikitika kumpoteza Imelda Malata, mfuatiliaji wa jamii kutoka mkoa wa Iringa, wilaya ya Mufindi. Imelda alianza kujitolea na shirika la Raleigh Tanzania mwaka 2018 kama mfuatiliaji wa jamii yake katika mradi wa Uwajibikaji wa Jamii Kupitia Vijana. Alitumia fursa hii vizuri na kitaalamu, alifanya kazi kwa ukaribu na viongozi wa Kijiji cha Kinengembasi.

Imelda alikuwa mchapakazi, alikua akifanya ufuatiliaji katika mradi wa Tajirika na Kilimo. Alihakikisha kuwa mradi unakua endelevu na kuwafikia wakulima wadogo katika Kijiji chake, Kama mfuatiliaji wa jamii, aliamini kuwa sauti ya vijana inaleta mabadiliko makubwa. Aliweza kuunda kikundi kazi katika jamii yake na hii ni sehemu ndogo sana ya mafanikio aliyofanya kwa kutumia sauti yake yenye kuhamasisha ushirikishwaji na utekelezaji. Tunaamini angeweza kufanya mengi Zaidi ya hayo.

Mkurugenzi wa Raleigh Tanzania, Alistair Mackay anasema: “Imelda alikuwa kiongozi bora, alikuwa mfano bora kwa kila mtu karibu yake. Tunasikitishwa kumpoteza mtu aliyejituma na kujali, maombi yetu kwa ndugu na rafiki zake. Hapa Raleigh, atakumbukwa na kila mtu aliyemfahamu na kufanya nae kazi na atakumbukwa kwa mawazo yake chanya katika kazi alizofanya. Uwezo wake katika kazi ya kujitolea ilimhamasisha kila mtu. Imelda alikuwa mfano wa kuigwa kwa vijana wengi na ataendelea kuwa kwenye mioyo yetu.’’

Raleigh Tanzania na Raleigh International inatoa pole kwa familia nzima ya Imelda na Kijiji cha Kinengembasi.

English

We are deeply saddened to hear about the passing of Imelda Malata, a Community Monitor from Iringa, Mufindi district. Imelda began volunteering with Raleigh Tanzania in 2018 as a Community Monitor for our Social Accountability through Youth (SAY) project. She took on this position with pride and professionalism, working closely with community leaders in Kinengembasi village.

Imelda was a hardworking volunteer who co-led monitoring of the Tajirika na Kilimo project. She was working to ensure that TNK project remains sustainable and young local farmers in her community are well trained. As a Community Monitor, she believed young people’s voice is integral to leading change. Her successful establishment of a joint working group within her own community is just a small example of the impact she was making by using her voice to encourage positive and collaborative social action. We are sure she would have gone on to achieve so much more.

Raleigh Tanzania Director, Alistair Mackay said: “Imelda was a wonderful young leader, who inspired everyone around her. We are so saddened to hear of the loss of such a committed and caring young person, and our thoughts are very much with her family and friends. At Raleigh, she will be missed by everyone who knew and worked with her and will be remembered for her enthusiasm and positivity at all the events she attended. Her joyful and open-minded approach to volunteering was so motivating to be around. Imelda was a true role-model for all young community leaders, and she will always be in our hearts”.

Raleigh Tanzania and Raleigh International sends our condolences to Imelda’s family and the entire community of Kinengembasi.

Related posts

News and Updates
Youth Creating Lasting Change in their communities.
News and Updates
The role of Women in a Joint Working Group
News and Updates
Hygiene must be inclusive for all